MATATIZO YA KIIMANI ->

HUU NI USHIA -SURA YA KWANZA

Sura ya Kwanza
Maana ya 'Shia'
 
Swali: Nini maana ya neno 'Shia?'
Jibu: Neno "Shia" linatokana na neno "Mushaayea'it ambako maana yake ni kufuata.
S: Kwa nini Mashia wanaitwa kwa jina hilo?
J: Kwa sababu wanamfuata Sayyidna Ali (a.s.) na wazao wake watakatifu wa Mtume Muhammad (s.a.w.) yaani Ahlul-Bayt.
S: Nani amewapa jina hilo?
J: Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.) ndiye aliyewapa jina hilo kama ilivyoandikwa katika vitabu vya Kisunni na Kishia.
S: Mashia wangapi wako duniani?
J: Zaidi ya milioni mia moja (100,000,000),

HUU NI USHIA
Sura ya Kwanza
Maana ya 'Shia'
 
Swali: Nini maana ya neno 'Shia?'
Jibu: Neno "Shia" linatokana na neno "Mushaayea'it ambako maana yake ni kufuata.
S: Kwa nini Mashia wanaitwa kwa jina hilo?
J: Kwa sababu wanamfuata Sayyidna Ali (a.s.) na wazao wake watakatifu wa Mtume Muhammad (s.a.w.) yaani Ahlul-Bayt.
S: Nani amewapa jina hilo?
J: Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.) ndiye aliyewapa jina hilo kama ilivyoandikwa katika vitabu vya Kisunni na Kishia.
S: Mashia wangapi wako duniani?
J: Zaidi ya milioni mia moja (100,000,000),
S: Wanaishi katika nchi gani?
J: Mashia wametawanyika katika kila nchi ya Kiislamu na isiyokuwa ya Kiislamu, na wengi wao wako nchini Iraq, Iran, Lebanon, India, Pakistan, Indonesia, Afghanistan, Turkey, Umoja wa Falme za Kiarabu, Oman, Kuwait, Bahrain, n.k.
S: Je, wanayo serikali yao wenyewe?
J: Ndiyo wanayo, ni Serikali ya Iran.
S: Je, walikuwa nazo tawala zao hapo zamani?
J: Ndiyo, tawala nyingi walikuwa nazo, kwa mfano, tawala za Safawisya, Buwahyi, Idrisi, hamdani, Qajar, Fatimiy, n.k.
S: Mashia wanao Maulamaa (wanavyuoni wa dini)?
J: Ndiyo, wako wengi kama nyota, tangu zamani hadi sasa.
S: Je, Mashia wanavyo vitabu vilivyopigwa chapa na wao wenyewe?
J: Ndiyo, tena idadi ya vitabu hivyo ni kama mchanga.
S: Je, wanayo adabu njema ya kuishi pamoja na Waislamu wengine kwa udugu, mapenzi na ushirikiano?
J: Ndiyo, mifano ya maisha yao inaweza kuonekana kila mahali, pawe Baghdad, Tehran, Cairo, Damascus au Beirut, n.k. Mashia na Masunni wanaishi pamoja kama ndugu.
S: Eti Mashia huwahesabu Waislamu wengine kuwa ni makafiri?
J:   Huu ni uzushi na uwongo usio na msingi uliobuniwa na wafitini.
S:   Je, ni kweli kuwa wao huwaita masahaba wa Mtume Mtukufu 'makafiri' na huwalaani?
J: Huu pia ni uzushi na uwongo unaoenezwa na wale ambao wanataka kuleta ugomvi baina ya Waislamu.
S: Je, ni kweli kuwa wao huyasujudia masanamu?
J: Huu ni uwongo na tuhuma tu. Inaruhusiwa kusujudu juu ya ardhi tu, au juu ya kile kinachoota humo ikiwa tu hakiliwi au hakivaliwi.
S: Kwa nini Mashia wanaitwa Ja'fari?
J: Kwa sababu Imamu wa sita Ja'far Sadiq (a.s.) alieneza kwa wingi sana mafundisho ya Qur'an na Mtukufu Mtume (s.a.w.), hata kwamba hadithi nyingi (zinazopatikana katika Shia), Tafsiri, Fiqhi
na maarifa mengineyo yanatoka kwake.
 

[ Umetembelea mara ngapi: 162]

Maoni ya watumiaji

commentName
Barua pepe
Matni ya barua
Namba ya Usalama